Mkuu wa Idara ya Utumishi na Utawala Ndugu. David Rwazo kwa niaba ya Mkurugenzi Jana March 12, 2025 aliongoza kikao cha tathimini ya Utekelezaji wa Shughuli za lishe kutoka Sekta mtambuka kwa kipindi cha robo ya robo ya kwanza (July-Septemba 2024/2025) na ya pili (Oktoba-Desemba 2024/2025m).
Kikao hicho kilipokea taarifa za utekelezaji wa afua za lishe kama vile upimaji wa kiwango cha madini joto katika Chumvi zinazouzwa sokoni, mahudhurio ya Wazazi kiliniki, Ugawaji wa vidonge vya kuongeza damu ( IFA) kwa Wajawazito, maadhimisho ya Siku ya afya na lishe ya Mtaa, na ugawaji wa Matone ya Vitamins A kwa Watoto.
Aidha kikao hicho kilijadili mikakati ya Shule za Msingi na Sekondari kwa Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula Shuleni kwa kuhamasisha Wazazi, Wadau na Wanafunzi kushiriki stadi za kilimo kwa Shule zenye maeneo ya kulima ili kuendelea kukuza viwango vya ufaulu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa