Wakazi wa manispaa ya kigoma ujiji wametakiwa kutunza mbiundombinu iliyopo na inayotarajiwa kujengwa kwa lengo la kukuza mji .jana may 31, 2018
Wameyaongea hayo watumishi wa benki ya dunia(World Bank) walipokuwa katika ziara ya kukagua miradi waliyoifadhili ikisimamiwa na Tanzania Strategic Cities Project(TSCP),na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) ambapo wamezungukia miradi mbali mbali ikiwemo barabara ya ya lami iliyojengwa kwa kiwango cha lami, mfereji wa maji NHC Katubuka, mfereji wa Rubengela, jengo la stendi kuu ya mabasi na vyoo katika standi hiyo,na ukaguzi wa dampo la msimba,
Watumishi waliokuwa katika ziara hiyo kutoka benki ya dunia(World Bank) ni Eng.Msiyangi Muindi, Mr. Mchalo Ignas, Mwakiluma Nkundwe, na ambapo watumishi kutoka wizarani alikuwa Eng. Ezrom(kwa jina moja) pamoja na Beatrice Mchome, Mkandarasi wa miradi hiyo Eng Jovine Ndyetabula, Mkurugenzi wa Manispaa, Baadhi ya wakuu wa idara na watumishi.
Wakiwa katika ziara hiyo walitoa ushauri mbalimbali katika miundombinu waliyoikagua kama vile utunzaji wa miundombinu hiyo ikiwa ni kusafisha mitalo katika barabara, kutotupa taka ovyo kwa mitalo hiyo kwa barabara ya Rusimbi, lakini pia waliweza kutoa pongezi kwa ujenzi uliofanyika mfereji wa Rubengela kutokana na jinsi mmomonyoko uliathiri eneo la shule ya msingi hata kupelekea baadhi ya miti kukatwa pasipo uhiari, ambapo wametoa ushauri katika eneo hilo kujengwa ukuta ili kuleta usalama kwa watoto wa shule na kupanda nyasi kwa lengo la kuboresha mazingira.
Na wakiwa katika stendi kuu ya Mabasi Masanga waliweza kujiridhisha na ujenzi unaoendelea wa jengo la ghorofa moja, ambapo jengo hilo litakuwa na ofsi ya msimamizi mkuu wa stendi,hotel, maduka, kituo cha polisi pamoja na huduma mbalimbali, wakiwa katika stendi hiyo waliwezakukagua ujenzi wa vyoo unaoendelea , ukaguzi wa ofsi za kukatia tiketi ambapo walimtaka mkurugenzi aanze kuruhusu kufanyia kazi kwa kuruhusu wafanyabiashara kuingia nao kwa mkataba rafiki utakao wanufaisha wafanyabiashara pamoja na halmashauri husika na walimtaka mhandisi kuweka taa mbili zilizopelea mbele ya ofsi hizo za kukatia tiketi ambapo aliahidi kulishugulikia ndani ya siku chache.
Baada ya hapo watumishi hao walimalizia ziara yao kwa kutembelea dampo la Msimba ambapo walijiridhisha kwa miundombinu iliyojengwa kwa majengo mawawili ya walinzi , eneo la ukarabati wa magari, na eneo la kumwaga taka linaloendelea ambapo wameshauri kujenga eneo kwa uzuri na kulaza karatasi zenye ubora zitakazo dhibiti kusambaa kwa sumu ardhini ambapo inaweza kuleta madhara kwa aldhi ya wakazi wa msimba ikiwemo taasisi ya shule iliyopo jirani na dampo hilo.
Watumishi hao wamesema wananchi ambao walioathirika katika barabara ya Rusimbi ambao nyumba zao zimepata nyufa halmashauri ifanye makubaliano mazuri na watumishi hao ili waweze kuendelea kuishi kwa uzuri.
Aidha mtumishi kutokea TAMISEMI Beatrice Mchome amewashukuru watumishi kutokea Banki ya Dunia na kusema watahakikisha yale wale walioambiwa kufanyia kazi watahakikisha wanayafanyia kazi na kusema watafatilia katika halmashauri kuhakikisha walioathirika na zoezi hilo wanarudi katika hali yao kwa uzuri.
Naye mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji amewashukuru pia wakaguzi hao na kusema ushauri huo wataufanyia kazi kwa ushauri wa stendi kuu katika kuingia mikataba na wafanyabiashara, kuunda kamati za usafi katika ya Rusimbi kwa lengo la kukuimarisha afya za wakazi na watumiaji wa barabara hiyo na katika kupanda miti na nyasi shule ya msingi ya Kigoma.
Wakaguzi hao walimaliza ziara yao saa tisa na nusu na kuwaaga kamati nzima ya ukaguzi kwa kuendelea kusimamia miradi hiyo na kusema wao wanaendelea na ziara maeneo mengine.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa