Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Ndugu. Ramadhani Kailima amewataka Watanzania kujitokeza kwa Wingi katika zoezi la uboreshaji wa daftari la Wapiga kura linalotarajiwa kuzinduliwa Mkoani Kigoma July 1, 2024.
Mkurugenzi huyo ameyasema hayo Mapema Leo May 29, 2024 alipokuwa akiongea na vyombo vya habari katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma huku akisema Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (MB).
Amesema siku ya uzinduzi ndiyo siku ambayo pia uboreshaji utaanza Mkoani Kigoma na kuendelea katika mikoa mingine ya Katavi, Rukwa na Tabora ambapo kwa kila Kituo zoezi lifanyika kwa mda wa Siku saba.
Mkurugenzi huyo ameendelea kusema katika uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura Nchini Tume huru inatarajia kuandikisha Wapiga kura wapya Zaidi ya Million tano (5, 586, 433), Wapiga kura wanaotarajia kuboresha taarifa zao zaidi ya Million nne (4, 369, 531) na baada ya uboreshaji Tume huru inatarajiwa kuwa na Daftari litakalokuwa na jumla ya wapiga kura zaidi ya Million thelathini na nne (34,746,638).
Aidha amesema Mkoani Kigoma Tume inatarajia kuandikisha wapiga kura wapya 224,355 katika vituo zaidi ya elfu moja (1,162) ikiwa ni ongezeko la 21% na baada ya uandikishaji Mkoa wa Kigoma utakuwa na wapiga kura 1,267,636.
Pia amesema Tume huru imefanya usanifu na kuboresha Mfumo wa Uandikishaji wa Wapiga Kura ambapo Watu watakuwa na uwezo wa kuboresha taarifa zao kupitia simu za Mkononi kupitia mfumo wa Voters Registration System-VRS.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa