Na Mwandishi Wetu
Viongozi wa dini jana Desemba 08, 2022 wametakiwa kuendelea kukemea vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika jamii ikiwa ni katika kuadhimisha siku kumi na sita (16) za kupinga ukatili wa Kinjisia
Aliyasema hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Ndugu. Albert Msovela Gabriel Alipokuwa Mgeni rasmi katika Kongamano la kupinga vitendo vya ukatili vya Wanawake na Watoto lililoandaliwa na shirika la Norwegian church Aid(NCA)
Alisema katika kutokomeza vitendo vya ukatili Viongozi wa dini hawana budi kutumia Maandiko Matakatifu kutoka katika Biblia na Quran kwa lengo la kukemea Mila na Desturi potofu za Kupinga Vitendo vya ukatili
Aidha aliwataka Wananchi kuwapuzia Waganga wa Jadi wanaokuwa na masharti yanayochochea vitendo vya ukatili kama vile mauaji kwa watu wenye ulemavu, ubakaji pamoja na Vitendo vya ulawiti
Alihitimisha kwa kuwataka Wananchi kuendelea kufichua vitendo vya ukatili na kuzitaka Taasisi za Sheria na vyombo vya habari kuendelea kuelimisha jamii na kuripoti matukio hayo kutokana na athari zitokanazo na vitendo hivyo
Akiwasilisha taarifa katika Kongamano hilo Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kigoma Ndugu. Petro Mbwaji Alisema tayari askari wa Jeshi la Polisi themanini na Saba (87) wamejengewa uwezo katika kushughulikia vitendo hivyo
Aliendelea kusema Walimu wa Unasihi Mashuleni Mia nane themanini na nane (888) wamejengewa na kupatiwa mafunzo na kujengewa uwezo namna ya Kushughulikia vitendo vya ukatili
Alisema vituo vinne (04) vya Mkono kwa Mkono vimejengwa kwa lengo la kurahisishwa Mhangwa wa vitendo vya ukatili kupatiwa huduma hiyo katika Wilaya ya Kibondo, Kakonko, na Hospitali ya Rufaa ya Maweni
Mratibu wa masuala ya Ukatili wa Kijinsia kutoka Shirika la Norwegian Church aid Bi. Zaria Mwenge alisema Shirika hilo limeendelea kutoa elimu kwa Wanawake na Watoto juu nnamna ya kupinga vitendo hivyo huku likiwajengea uwezo wanawake katika Mradi ya Maendeleo
Mkurugenzi wa kurugenzi ya Uchungaji Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tec) Fr. Florence Rutauywa na Shekhe wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke wakichangangia katika Kongamano hilo wakisema vitabu Vitakatifu vikekataza Vitendo vya ukatili kutokana na Sheria na Amri Kumi za Mungu
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa