Na Mwandishi Wetu
Ikiwa ni maadhimisho ya Siku 16 za kupinga ukatili wa Kijinsia Viongozi wa dini na Kimila Jana Novemba 27, 2025 walikutana katika ukumbi wa Ndela uliopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kujadili na kutokomeza vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikijitokeza ndani ya Jamii hasa kwa Wanawake na Watoto.
Afisa Maendeleo ya Jamii Ndugu. Jabir Majira aliwataka Viongozi hao kuendelea kuelimisha na kusimamia ili kuhakikisha kunakuwa na Jamii yenye maadili.
Aidha aliwataka kuielimisha Jamii katika malezi na maadili yanayofaa na kuendelea kutoa taarifa katika Mamlaka husika pindi vitendo vya ukatili vinapotokea.
Akichangia katika kikao hicho Mchungaji Godfrey Malela alisema kwa sasa Jamii inakabiliwa na Changamoto kujifunza utamaduni wa nje kupitia Mitandao ya kijamii huku akizitaka familia kuwa na vikao vya mara kwa mara kuzungumzia malezi na udhibiti wa Vitendo vya Ukatili.
Kauli mbiu ya Mwaka huu " Tuungane kutokomeza Ukatili wa Kijinsia Mtandaoni".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa