Na Mwandishi Wetu
Viongozi wa elimu Manispaa ya Kigoma/Ujiji leo Septemba 29, 2022 wamefanya kikao cha siku moja cha kujadili namna ya uboreshaji na uwekaji mikakati ya ukuzaji taaluma huku wakizindua miongozo na mikakati ya kuboresha elimu ya Msingi na Sekondari
kikao hicho kilichofanyikia ukumbi wa Shule ya Sekondari Buronge kimehusisha Maafisa elimu ngazi ya Halmashauri, Maafisa elimu Kata, Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari
Akifungua Mkutano huo Afisa elimu Sekondari Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Lawi Kajanja amewataka Maafisa elimu Kata na Wakuu wa Shule kusimamia kikamilifu suala la ufundishaji na ujifunzaji kwa kuzingatia miongozo na sera ya elimu Nchini
Aidha amewataka viongozi hao kusimamia suala la Ukuaji wa taaluma na maadili ili kuzalisha na kuandaa wataalamu waliobora katika fani mbalimbali
Naye Katibu Msaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC) Ndugu. Obadia Makoko amesema katika taasisi za elimu kumekuwa na vitendo visivyo vya maadili kama vile utoro wa baadhi ya Walimu kazini, kutofundisha vipindi na baadhi ya vitendo vya ukatili vinavyoweza kusababisha Matokeo mabaya katika maendeleo na mitihani ya Wanafunzi hali inayowezeza kusababisha kuzalisha wataalamu na jamii isiyo na maadili
Amewataka Viongozi hao kutofumbia macho vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu kazini na kusimamia maadili ya kazi kikamilifu kwa kushughulikia katika nafasi zao pale vitendo hivyo vinapojitokeza ili kuhakisha ukuaji wa elimu katika Manispaa hiyo
Aidha amesema kuvunjwa kwa maadili ya kazi kwa Walimu wawapo kazini kunaweza kupelekea adhabu mbalimbali ikiwemo kupata barua za onyo, kuzuia ongezeko la mshahara, kushushwa kwa ngazi ya mshahara au kufukuzwa kazi
Katika kikao hicho Wataalamu hao kwa pamoja wameweka mikakati ya kuhakikisha wanasimamia suala la ufundishaji kwa Walimu, kuzingatia maadili ya kazi na kuimarisha Ulinzi na Usalama wa ujifunzaji Mwafunzi
Katika kikao hicho miongozo iliyozinduliwa ni pamoja na muongozo wa uteuzi wa Viongozi wa elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikoa , mwongozo wa Changamoto katika uboreshaji wa elimu Msingi na Sekondari na nini kifanyike, na muongozo wa kitabu cha kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji katika ngazi ya elimu msingi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa