Na Mwandishi Wetu
Wataalamu wa afya Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo Novemba 14, 2025 wametoa elimu ya udhibiti na upimaji wa Magonjwa yasiyoambukiza bure kwa Watumishi na Wananchi wa Manispaa hiyo.
Zoezi la utoaji elimu na upimaji limefanyika katika viwanja vya Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ikiwa ni wiki ya maadhimisho ya magonjwa yasiyoambukiza kuanzia Novemba10-15, 2025.
Wataalamu hao wametoa elimu ya mtindo wa maisha ikiwemo ulaji, kufanya mazoezi na upimaji wa afya mara kwa mara.
Vipimo vilivyotolewa ni vya ugonjwa wa Kisukari, Shinikizo la damu, Upimaji wa uzito na urefu pamoja na elimu ya lishe bora.
#AfyayakoMtajiwako.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa