Na Mwandishi Wetu
Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji imetoa vitambulisho vya Wazee Mia tano sitini na nane (568) kwa Baraza la Wazee la Manispaa hiyo vitakavyosaidia upatikanaji wa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za Matibabu ya bure
Vitambulisho hivyo vilitolewa siku ya Ijumaa Agost 26, 2022 na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Ndugu. Athumani Msabila huku akianza na Kata sita (06) kati ya Kata Kumi na Tisa (19) zilizopo katika Manispaa hiyo
Mkurugenzi huyo alisema tayari Wazee Elfu moja mia mbili themanini na tisa (1289) tayari wametambuliwa katika kata mbalimbali zilizopo katika manispaa hiyo na zoezi la kuwatambua bado linaendelea
Mkurugenzi huyo aliitaka jamii kuendelea kuwaheshimu wazee katika Maeneo mbalimbali kutokana na mchango wao wa kulihudumia Taifa katika sekta mbalimbali huku akizitakà Taasisi za Serikali na zisizo za Serikali kuwapa kipaumbele katika huduma mbalimbali kutoka a na vitambulisho hivyo ambavyo watavitumia
Aidha Mkurugenzi huyo alisema vitambulisho vya Wazee vinaendelea kuzalishwa huku akisema Wazee wote waliotambuliwa watapewa vitambulisho hivyo kwa lengo la kuwasaidia kutumia katika huduma mbalimbali
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mzee Zuberi Kisongo alimshukuru Mkurugenzi huyo kwa kuwathamini Wazee katika vitambulisho vilivyotolewa ambavyo vitawasaidia kupata huduma za bure na haraka katika taasisi mbalimbali
Alisema tayari Baraza la Wazee limeweka utaratibu wa kupita kila Kata kwà ajili ya kugawa vitambulisho hivyo ambavyo wamekabidhiwa tayari
Wazee walioanza kupatiwa vitambulisho vya wazee ni ķutoka kata sita (6) ikiwemo kata ya Kigoma, Bangwe, Mwanga Kusini, Machinjioni, Rubuga na Kata ya Kitongoni
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa