Na Mwandishi Wetu
Wazazi na Walezi wenye Watoto chini ya Umri wa Miaka mitano (05) wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Ofisi za Watendaji Kata na Katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa lengo la kusajili na kupata vyeti vya kuzaliwa
Ameyasema hayo Waziri wa Katiba na Sheria Nchini Tanzania Dr. Pindi Chana Leo Octoba 3, 2023 alipokuwa akizindua Mpango wa Kusajili na Kutoa Vyeti vya kuzaliwa chini ya Miaka 5 Mkoani Kigoma
Katika Uzinduzi huo uliofanyikia Uwanja wa Mwanga Community Centre Manispaa ya Kigoma/Ujiji Waziri amesema zoezi hilo la Usajili na Kutoa vyeti vya kuzaliwa litafanyika katika Ofisi za Watendaji Kata na vituo vya kutolea afya huku akiwataka Wananchi wenye watoto wenye Umri huo kujitokeza
Akitoa Salamu katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kali (Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa) amesema zaidi ya Watoto laki tatu ( 396,000) wanatarajiwa kusajiliwa na kupata vyeti vya kuzaliwa
Zaidi www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa