Na Mwandishi Wetu
Wajasiriamali na Wafanyabiashara wa Soko la Masanga waliopisha Ujenzi katika Soko la Mwanga Jana July 11, 2022 waliupongeza Uongozi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa utaratibu uliotumika wa kuhakikisha wanapata maeneo ya kufanyia biashara zao
Waliyasema hayo katika Mkutano uliofanyika na Meya wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mhe. Baraka Naibuha Lupoli katika Soko hilo jipya la Masanga wakati wa uhakiki zoezi la ugawaji wa maeneo kwa Wajasiriamali hao
Mwenyekiti wa Wauza Nyanya na Mboga Mboga Bi. Mayase Hamisi na Mwenyekiti wa Wauza Viatu na Ndala(Yebo Yebo) Daudi Makota walisema Viongozi wa Manispaa kupitia Wataalamu awali waliandika majina ya Wajasiriamali Wote waliokuwa Soko la Mwanga kabla ya kupisha Ujenzi na majina hayo ndio yaliyotumika kuhakikisha kila mlengwa ana nufaika na soko hilo jipya la Masanga
Naye Meya wa Manispaa hiyo aliwapongeza wajasiriamali hao kwa kupisha Ujenzi wa soko la Mwanga utakaojengwa Kisasa huku akisema uboreshaji wa soko hilo la Masanga utaendelea kwa kujenga Shedi (Vizimba) vitakavyosaidia wajasiriamali hao kujikinga na jua na katika kipindi cha Mvua
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa