Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Nyakoro Sirro amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo kusimamia zoezi la utoaji dawa kinga za minyoo ya tumbo na kichocho kwa Watoto wenye umri wa kwenda Shule kuanzia miaka 5-14.
Maelekezo hayo ameyatoa Leo Novemba 21, 2025 alipokuwa akifungua kikao kazi cha kujadili na kupanga utekelezaji wa zoezi la umezaji wa dawa kinga za minyoo ya Tumbo na kichocho kilichofanyika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
Amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha Watoto wa umri huo wanatambuliwa na kupatiwa kinga tiba ili kupunguza magonjwa ya mara kwa mara ambayo husababisha Ulemavu wa kudumu, vifo na umasikini.
Awali akizungumza Mratibu wa Magonjwa ya kichocho na minyoo ya tumbo kutoka Wizara ya afya Ndugu. Godfrey George Ngariba amesema Serikali imekuwa ikiwajali Wananchi kwa kutoa kinga kwa magonjwa yasiyozuilika huku akisema zoezi la utoaji dawa kinga linagharamiwa na fedha za ndani(Serikali Kuu).
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dr. Damas Kayera amesema dawa kinga znatarajia kutolewa mapema Mwezi January 2026, kwa Watoto 797,119 wa Mkoa huo wenye umri wa kwenda Shule.
Amesema zoezi hili litahusisha umezaji dawa ya Albendazole pamoja na Preziquentel ikiwa ni dawa salama kwa matumizi ya Watoto.
Kikao kazi hicho kimehudhuriwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa, Wataalamu kutoka Wizara ya Afya, Mganga Mkuu wa Mkoa,Wakurugenzi wa Halmashauri, Waganga Wakuu wa Halmashauri, Maafisa elimu, Waratibu wa Mgonjwa yasiyopewa kipaumbele na Wafamasia wa Halmashauri.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa