Na Mwandishi Wetu
Wakuu wa idara na Vitengo Manispaa ya kigoma/Ujiji wametakiwa kujenga Mahusiano mazuri kwa kuwa na upendo mahala pa kazi na watumishi wanaowaongoza
Yamesemwa hayo na Mwezeshaji wa Mafunzo ya Malezi, Unasihi na Ulinzi wa Mtoto Kitaifa Ndugu. Cornel Kisinga katika Mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la UNICEF la kuijengea uwezo Kamati tendaji ya Halmashauri (CMT) juu ya Ulinzi na Usalama wa Watoto na Wanawake iliyofanyika Leo July 21, 2022 katika Ukumbi wa Manispaa hiyo
Amesema katika kuhakikisha malengo ya Taasisi yanafikiwa Wakuu wa Idara na Vitengo wana wajibu wa kusimamia na kuhakikisha Watumishi wanaowaongoza wanajua malengo ya idara zao , Matumizi sahihi ya Rasilimali, na kujua Sheria zinazoongoza utendaji wao
Aidha amesema upendo baina ya watumishi ni muhimu mahala pa kazi na nje ya maeneo ya kazi ili kusaidiana katika mambo mbalimbali jambo linalokuza ufanisi wa kazi na kufìkia malengo yaliyokusudiwa
Mratibu wa Mafunzo ambaye pia ni Afisa Ustawi wa jamii Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Agnes Punjila amewataka Viongozi hao kuhakikisha wanawalinda Watoto na Wanawake katika vitendo vya ukatili ambavyo vimekuwa vikijitokeza katika Jamii huku wakiaswa kuwa na mda wa kutosha wa kukaa ili kujadili changamoto na Mafanikio ya familia
Mkuu wa idara ya Elimu Sekondari Ndugu. Kanjanja Lawi amesema Mafunzo hayo ni mhimu kwa watumishi wote ili kukuza utendaji mahala pa kazi, kukuza mahusiano na namna ya kushughulikia migogoro
Mada nyingine iliyowasilishwa ni pamoja na Msaada wa Kisaikolojia na changamoto za Kisaikolojia kama vile Afya ya akili, na namna ya kushughulikia msongo wa mawazo mahala pa kazi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa