Na Mwandishi Wetu
Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari wametakiwa kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili vinavyotokea Mashuleni kila Mwezi na kueleza hatua zilizochukuliwa kwa kila tukio na kuripoti kwa Mamlaka zinazoshughulikia vitendo hivyo ikiwemo Jeshi la Polisi na Ustawi wa jamii
Maagizo hayo yametolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi Leo July 14, 2022 wakati akifungua Mafunzo ya Siku Saba (7) yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wakishirikiana na UNICEF kwa Walimu Wakuu, na Walimu Wanasihi juu ya Malezi, Unasihi na Ulinzi wa Mtoto awapo Shuleni
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema vitendo vya ukatili vimekuwa vikitokea ndani ya jamii ikiwemo Mazingira ya Shuleni vikisababishwa na Watu wa Karibu wanaowazunguka Watoto na Watoto Wenyewe jambo linaloathiri tendo la Ufundishaji na Ujifunzaji
Kaimu Mkurugenzi huyo amesema " Ni lazima tukomeshe vitendo vya ukatili kwa aina zake bila kujali nani kasabibisha, hivyo niwaagize Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari katika taarifa zenu za kila Mwezi Mnazoziwasilisha hakikisha unaambatanisha na kesi za ukatili zilizopokelewa na namna zilivyoshughulikiwa kwa kila Shule "
Afisa Ustawi wa Jamii ambaye ni Mkufunzi wa Mafunzo hayo Bi.Agnes Punjila amesema katika ulinzi wa Mtoto Shuleni Mwalimu ana wajibu wa kuhakikisha Ukuaji wa Mtoto unakuwa Kimwili, Kiakili, kihisia, Kijamii na kwa kuzingatia Watoto Wenye Mahitaji Maalumu
Aidha amewataka Walimu Wanasihi Mashuleni kutumia mbinu tofauti tofauti katika kunasihi Wanafunzi kwa lengo la kuibua na kushugulikia na matatizo ya Ukatili ikiwemo njia ya Mwalimu (Mnasihi) kuwa kitovu cha Unasihi , Mnasihi kuwa chanzo cha Unasihi na Njia Mseto
Afisa elimu ya Watu Wazima Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Mkufunzi wa Mafunzo hayo Ndugu. Cornel Kisinga amewataka Walimu kutenga Ofisi Maalumu za Unasihi na kushughulikia ukatili Mashuleni kwa lengo la kuwafanya Wanafunzi kujiamini katika kueleza changamoto zao
Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwananchi Ndugu.Maxminus Wabera ambaye ni Mshiriki wa mafunzo akizungumza mara baada ya Ufunguzi amesema Mafunzo hayo yatawanufaisha Kujenga Mahusiano mazuri Kati ya Wanafunzi na walimu katika kutokomeza vitendo vya ukatilinna hatimaye kuinua Taaluma na baadhi ya Wakuu wa Shule tayari watenga ofisi za Unasihi na Shule zingine utekelezaji unaendelea
Utafiti wa Taasisi ya Haki Elimu Tanzania mwaka 2020 ulionesha kuwa asilimia themanini na tisa (89%) ya vitendo vya kupiga na maumivu ya kimwili vimekuwa vikifanyika mashuleni na utafiti huo ukieleza vitendo vingi hufanyika zaidi kwa shule za vijijini
Kwa mjibu wa Tafiti iliyofanywa na Serikali mwaka 2009 juu ya hali ya ukatili na kutolewa mwaka 2011 ilionyesha wasichana 3 kati ya 10 na Mvulana 1 kati ya 7 walifanyiwa ukatili wa Kingono na asilimia 71 ya Wavulana na asilimia 72 ya wasichana walifanyiwa ukatili wa kimwili na utafiti huo ulibainisha kuwa asilimia sitini (60%) ya ukatili dhidi ya watoto hufanyika majumbani huku asilimia arobaini (40%) ukifanyika mashuleni
Picha na video zaidi tembelea Maktaba ya Tovuti www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa