Na Mwandishi Wetu
Mafunzo ya mpango wa kuhamasisha jamii ya kuweka akiba na kuwekeza yamefunguliwa Manispaa ya Kigoma/Uji ji kwa lengo la kuwawezesha wanufaika wa TASAF kuwekeza kupitia taasisi za kifedha (Vikundi) ili kuinua vipato vya kaya na kuondokana na umasikini
Mafunzo hayo yamefunguliwa leo Desemba 1, 2021 katika ukumbi wa Manispaa hiyo ambapo Wataalamu mbalimbali wanapatiwa mafunzo ya siku tano (05) ya nadharia na vitendo kwa lengo la kuelimisha na kuhamasisha uundaji wa vikundi vya kuweka akiba katika mitaa
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi amewataka wawezeshaji hao watakaopatiwa mafunzo kutoa elimu kwa weredi kwa walengwa wa TASAF namna na hatua ya kujiunga katika vikundi vya kuweka na kukopa huku akiwataka kujenga ushirikiano kwa viongozi wa Kata na Mitaa na kuhakikisha wanufaika wanajiunga kwa wingi
Mmoja wa wawezeshaji Kitaifa kutoka TASAF Makao makuu Ndugu. Geradi Adolfu amesema katika kipindi cha TASAF Awamu ya tatu kaya Maskini walipata mafunzo ya Ujasiriamali na mbinu za kuunda vikundi endelevu vya kuweka akiba ambapo jumla ya Vikundi elfu ishirini na tatu mia sita kumi na nane (23,618) vyenye jumla ya wanachama laki tatu kumi na tisa mia tisa arobaini (319,940) viliundwa kwa Halmashauri sabini na nane (78) kutoka Tanzania Bara, Unguja na Pemba na wameweza kukusanya akiba ya Shilingi Bilion 5.9 kati ya hizo billion 2.5 zimekopeshwa kwa wanachama riba nafuu
Naye Mratibu TASAF Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Izack Vyabandi amesema kwa mwaka wa fedha 2014/2015 hadi 2020/2021 Halmashauri hiyo imeshapokea kiasi cha fedha jumla ya Billion kumi na moja million mia sita ishirini na tano laki nane hamsini na nne elfu mia mbili kumi na tisa (Tsh 11,625,854,219.74/=) na kuwafikia walengwa wa kaya Maskini kwa vipindi thelathini na moja (31) vya malipo
Ameendelea kusema manispaa ya Kigoma/Ujiji ina jumla ya Kaya elfu saba mia tisa hamsini na nne (7,954) ambazo ni wanufaika wa TASAF na inatarajia kuunda vikundi mia tano thelathini (530) vyenye idadi ya wanakukikundi kati ya kumi (10) hadi kumi na tano (15)
Aidha amesema mpango wa kunusuru kaya Maskini Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika kipindi cha TASAF awamu ya tatu kaya elfu sita mia tisa hamsini na mbili (6,952) zinamiliki aina mbalimbali za mifugo na kujishughulisha na shughuli za uzalishaji mali
Mmoja wa wawezeshaji ambaye amehudhuria mafunzo hayo ambaye ni Mtaalamu wa Kilimo Ndugu. Haruna Mtandanyi amesema elimu watakayoipata itawawezesha kwenda kuhamasisha uundaji wa vikundi vya kuweka na kuwekeza ili kuongeza kipato, fursa na kuinuka kiuchumi kwa kaya Maskini
Mpango wa kunusuru kaya Maskini Manispaa ya Kigoma/Ujiji unatekelezwa katika mitaa arobaini na tisa (49) kati ya Mitaa sitini na nane (68) sawa na asilimia sabini (70%) ya utekelezaji kwa kaya maskini
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa