Na Mwandishi Wetu
Viongozi wa elimu na Walimu wa MEMKWA Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamepata mafunzo ya Siku mbili (02) kuhusu Mfumo wa kidigitali wa taarifa za Shule(SIS).
Mafunzo hayo yalianza Jana Oktoba 14, 2025 yakifadhiliwa na Shirika la Kimataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) Kwa Waratibu elimu Kata, Walimu Wakuu, na Walimu wa madarasa ya MEMKWA.
Akizungumza katika mafunzo hayo Mwezeshaji na Afisa Elimu Watu wazima Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Cornel Kisinga amesema mafunzo ya mfumo wa taarifa za Shule(SIS) unalenga kuinua upatikanaji wa taarifa za Shule zinanasosaidia kuboresha Utawala wa Shule kwa kuhakikisha taarifa muhimu zinapatikana.
Amesema mfumu huo wa kidigitali unasaidia uwepo wa takwimu sahihi za orodha ya Wanafunzi na taarifa zao, Orodha ya Walimu na taarifa zao, Mahudhurio ya Walimu na Wanafunzi, taarifa za matokeo ya mitihani na Maendeleo ya Wanafunzi, usimamizi wa rasilimali za Shule, na taarifa mbalimbali za Wadau wa elimu.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa