Na Mwandishi Wetu
Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari Manispaa ya Kigoma/Ujiji ambao ni wasimamizi wa maadili leo April 24, 2024 wamepata Mafunzo ya kuendesha clabu za maadili kwa Wanafunzi.
Mafunzo hayo yametolewa na Wataalamu kutoka Tume ya Sekretarieti ya Viongozi wa Umma kanda ya Magharibi katika Ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Awali akifungua mafunzo Mkuu wa Idara ya Rasilimali Watu Ndugu. Idrisa Naumanga kwa niaba ya Mkurugenzi amewataka Walimu hao kuzingatia Mafunzo na kuwa mabalozi katika kuelimisha, kuhamasisha, kushirikisha Wanafunzi, Walimu na jamii kuhusu maadili yanayokubalika.
Aidha amewataka kuanzisha clabu za maadili za Wanafunzi kwa lengo la kufundisha matendo mema, kusema ukweli, Uwazi, kupenda haki, Msimamo, misingi bora ya maadili, na kuwa na Taifa lenye Watu wenye maadili.
Naye Afisa Maadili Mwandamizi kutoka Tume ya Sekretarieti ya Viongozi wa Umma kanda ya Magharibi Bi. Halima Mnenge amesema katika Mafunzo hayo watapitia muongozo wa kuanzisha na kuendesha Clabu za maadili katika Shule za Msingi, Sekondari na vyuo vya elimu Tanzania.
Amewataka Walimu kuwajengea uwezo Wanafunzi kutoa taarifa kwa vitendo visivyo vya maadili vinavyofanyika katika jamii.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa