Na Mwandishi Wetu
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Shule Bora OR- TAMISEMI Bi. Adelaida Pangani amewataka walimu kuzingatia mafunzo yenye lengo la kuinua ubora wa elimu Nchini
Aliyasema hayo Jana Desemba 13, 2022 katika Mafunzo ya siku mbili (02) ya Walimu Kazini (MEWAKA) yanayoendelea katika Shule ya Msingi Kigoma yakihusisha Watendaji Kata, Waratibu Elimu Kata, Walimu Wakuu, Walimu Wataaluma na Walimu Mahili wa Shule za Msingi zilizopo Kata za Kigoma na Bangwe
Alisema lengo la Mafunzo hayo ni kuwawezesha Walimu kuibua hadithi za mafanikio za kujifunza za mfano zinazopatikana miongoni mwao ili kutatatua changamoto za ujifunzaji na ufundishaji ili kuinua ubora wa elimu nchini
Aliwataka Wasimamizi wa elimu ngazi za Kata kila mtu kutekeleza wajibu wake kwa kuwashirikisha Wazazi na wadau mbalimbali wa elimu katika kukuza elimu Nchini
Mradi wa Shule bora umelenga kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira salama ya kujifunzia kwa Wanafunzi wote wa kike na wa kiume katika Shule za Serikali za Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK aid , gharama za mradi zikiwa ni Shilingi za Kitanzania bilion 271 na utafanya katika ngazi zote za mradi katika mikoa ya Kigoma, Katavi, Rukwa, Singida, Dodoma, Simiyu, Mara, Tanga na Pwani ambapo utafikia kikomo mwaka 2027
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa