Na Mwandishi Wetu
Viongozi na wadau wa elimu ngazi ya kata na Mitaa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wametakiwa kuihamasisha jamii kujiunga na Mpango wa elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA)
Yamesemwa hayo na Mwezeshaji wa mafunzo ya MEMKWA Kitaifa kutoka taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Dr. Sempeho Siafu Leo March 20, 2023 wakati wa mafunzo ya kuwajengea Walimu wa MEMKWA kufundisha Wanafunzi kwa tija
Mafunzo hayo yamefanyikia ukumbi wa Jengo la Chama cha Walimu (CWT) Kigoma yakihusisha Maafisa Watendaji Kata, Maafisa elimu Kata, Wenyeviti wa Serikali Za Mitaa, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Walimu wakuu na Walimu wa MEMKWA yakofadhiliwa na Shirika la UNICEF
Mwezeshaji wa mafunzo ya MEMKWA Kitaifa kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Bi. Oliver Kindole amesema elimu hiyo hufundishwa stadi za Kusoma, Kuandika na kuhesabu pamoja na Stadi za maisha, Falsafa ya Ujasiriamali, na stadi za ufundi kwa lengo la kuchangia Maendeleo ya Taifa pindi anapohitimu masomo
Amesema elimu ya MEMKWA hutolewa kwa kundi rika umri wa miaka 8-13 na kwa vijana walio na umri 14-18 na baadae hujiunga katika mfumo wa elimu rasmi kwa kufanya mtihani wa Darasa la nne na la Saba
Naye Afisa elimu Watu wazima Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Cornel Kisinga amesema Vituo vya MEMKWA vipo katika Shule zote za Msingi za Serikali zipatazo arobaini na tano (45) zilizopo katika Manispaa hiyo
Amesema jamii inapaswa kuhakikisha Watoto wote wanapata elimu pasipo kikwazo chochote ili kupunguza ongezeko la Watoto mtaani , kupunguza idadi ya Watu wasiojua Kusoma, Kuandika na kuhesabu, kupunguza ajira za utotoni na ukatili katika jamii
Tamko la Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Nchini inataka kupata idadi kubwa ya Watanzania walioelimika, Wanaopenda kujielimisha, ili waweze kuchangia Maendeleo ya Taifa na Serikali imetoa fursa kwa Watoto waliokosa elimu kupitia Mpango wa elimu ya Msingi kwa Watoto Walioikosa (MEMKWA)
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa