Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua ameyataka Mashirika yasiyo ya Kiserikali yenye kibali cha kutoa elimu ya Mpiga Kura kuendelea kuelimisha Jamii Kushiriki Uchaguzi Mkuu Oktoba 29, Mwaka huu.
Ameyasema hayo katika hotuba yake ya kufungua kikao cha robo ya Kwanza (Julai-Septemba) 2025 cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali Manispaa ya Kigoma/Ujiji iliyowasilishwa na Afisa Tawala Bi. Dorah Buzaire katika ukumbi wa Redcross.
Amewataka Wananchi kujitokeza kupiga Kura kwa kuchagua Rais, Wabunge na madiwani watakaongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Aidha ameyakumbusha Mashirika hayo kuwa ni kosa Kisheria kuonekana Shirika lenye kibali kutoa elimu ya Mpiga Kura kuchangia kibali hicho na Shirika jingine.
Aidha amesisitiza Mashirika hayo kuendelea kufanya kazi kwa kuzingatia kanuni na taratibu na kulinda maslahi ya Nchi ikiwa ni pamoja na kutii Sheria na kuheshimu Mila na desturi za Jamii za Kitanzania.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kelvin Mihambi amewataka Viongozi wa Mashirika kuendelea Kushirikiana katika kuwahudumia Wananchi katika katika Sekta za afya, elimu, kilimo, Mazingira, jinsia, na uwezeshaji wa Wanawake na Vijana.
Mwakilishi wa Baraza la Uratibu Mashirika yasiyo ya Kiserikali Mkoani Kigoma (NaCoNGO) Ndugu. Alex Izack Luoga amesema Mashirika yasiyo ya Kiserikali Manispaa ya Kigoma/Ujiji yataendelea kuendeshwa kwa uwazi na kushirikiana na Serikali katika kuwahudumia Wananchi.
Zaidi Bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa