Na Mwandishi Wetu
Katibu tawala wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Mganwa Nzota amekemea tabia za Wanachi wanaoharibu miundombinu ya nguzo na vibao vya anwani ya Makazi na kutumia kama vyuma chakavu.
Ameyasema hayo Leo March 13, 2024 wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mfumo wa anwani za makazi kwa Watendaji wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Mitaa katika ukumbi wa Redcross yanayotolewa na Wataalamu kutoka Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari.
Amewataka Watendaji wa Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa kushirikiana na Wananchi kuwabaini Waharifu na kuwachukulia hatua katika kuharibu miundombinu ya Postikodi.
Akiwasilisha mada Mtaalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi kutoka Wizara ya habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Ndugu. Charles Watson Gombo amesema lengo la zoezi hilo ni kusasisha taarifa na miundombinu iliyofanyika kwa kipindi kilichopita, kuhuisha na kukusanya taarifa mpya.
Amesema mafunzo hayo yanatarajia kufanyika kwa mda wa siku mbili (02) na zoezi la uhakiki wa taarifa ukifanyika kwa siku kumi na mbili kwa kushirikisha Viongozi hao na Wananchi katika mitaa sitini na nane (68) ya Manispaa hiyo.
Utambuzi na uwekaji wa Anwani za makazi Nchini ulifanyika na unafanyika kwa kutoa namba ya anwani (namba ya jengo, au kiwanja), majina ya barabara au kitongoji na postikodi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa