Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja amewataka Wananchi kutoa ushirikiano katika miradi inayotekelezwa katika Manispaa hiyo
Ameyasema hayo Leo July 13, 2023 katika kipindi cha #goodmorningkigoma kinachorushwa na radio joy 90.5
Mkurugenzi huyo ameeleza miradi inayotekelezwa na fedha kutoka Serikali Kuu na mapato ya ndani
Amesema kwa Sasa Halmashauri inatekeleza ujenzi wa Shule Mpya na madarasa kupitia mradi wa BOOST kwa gharama ya zaidi ya Billion moja (Tsh 1, 467, 200, 000/=) fedha kutoka Serikali Kuu, Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa unaoendelea Kata ya Kagera fedha kutoka Serikali kuu , Ujenzi wa ofisi za Kata ya Mwanga Kusini, Majengo na Buhanda, Ujenzi wa ofisi ya Kata Katubuka ukiwa umekamilika, na ujenzi wa Zahanati ya Machinjioni kupitia mapato ya ndani
Amewataka Wananchi kutoa taarifa sahihi pale ambapo miradi hiyo inapoharibiwa na kuhujumiwa ili kuhakikisha thamani ya fedha katika mradi inaonekana
Amehitimisha kwa kuwataka Wananchi kujitokeza na kushiriki katika Mwenge wa Uhuru utakaopokelewa August 22, Mwaka huu katika eneo la Shule ya Sekondari Buronge, eneo la miradi na katika eneo la Mkesha la Mwanga Community centre
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa