Na Mwandishi Wetu
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Kanali Michael Masala Ngayalina (ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe) amewataka wakazi wa Wilaya ya Kigoma kuzingatia usafi kutokana na uwepo wa wagonjwa wa Matumbo katika Wilaya hiyo
Kaimu Mkuu wa Wilaya huyo ameyasema hayo alipokuwa katika kikao cha Afya ya Msingi ya jamii kilichofanyikia Leo January 14, 2022 katika ukumbi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Amesema mapema mwezi January 2022, idadi ndogo ya Wagonjwa wa Matumbo walitibiwa katika zahanati na maeneo ya Kutolea huduma za Afya Manispaa ya Kigoma/Ujiji ambapo idadi hiyo imeongezeka hadi kufikia Wagonjwa kumi na nne (14) wengi wao wakiwa raia wa Nchi jirani, wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji eneo la Kibirizi na wengine wakitokea Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma
katika kikao hicho amewataka wakazi wa Wilaya ya Kigoma kuzingatia na kuchukua tahadhari ya Magonjwa hayo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananawa kwa maji safi na sabuni wakati wa kula na baada ya kutoka chooni, kuzingatia usafi wa vyakula na Maji, matumizi sahihi ya vyoo, na kujenga utamaduni wa kunawa mikono kila mara
Aidha amewataka Wataalamu wa afya na idara zingine kusimamia na kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa hayo katika mikusanyiko ya watu kwa njia ya vipeperushi , vyombo vya habari na matangazo ya sauti
Amehitimisha Kwa kuwataka wakazi wa Wilaya hiyo kuhakikisha wanafika katika vituo vya Kutolea huduma za Afya na kutoa taarifa Mara baada ya kuhisi dalili za Ugonjwa huo huku akisema tayari jitihada za kuwahudumia wagonjwa hao zinaendelea katika Zahanati ya Bangwe
Kikao hicho Kimehudhuria na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Kigoma, Wajumbe wa Kamati za Afya ngazi ya Jamii, Kamati ya Uchumi, elimu na Afya, Wataalamu wa Afya ngazi ya Wizara, Wataalamu kutoka KUWASA, na Mashirika ya Serikali na yasiyo ya Serikali
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa