Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Adengenye amesema Wananchi wa Mkoa wa Kigoma wamemkubali na kumuelewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassani kwa namna anavyotekeleza miradi ya maendeleo Mkoani humo.
Ameyasema hayo Leo Octoba 11, 2023 wakati wa Hafla ya Utiaji saini wa Mikataba mitatu ya Ujenzi wa meli katika Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria kwa gharama ya Zaidi ya Billion 630 uliofanyikia eneo la bandari ya Kigoma.
Katika Hafla amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuonesha kwa vitendo nia ya kufungua fursa Mkoani Kigoma kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Ujenzi wa miundombinu ya barabara ndani ya Mkoa, Ujenzi wa Reli ya Kisasa kipande cha SGR kilomita 506 kutoka Tabora hadi Kigoma, na Upanuzi wa Uwanja wa ndege kwa lengo la kutua masaa ishirini na nne.
Katika mikataba iliyosainiwa imehusisha Ujenzi wa kiwanda cha ujenzi wa meli (karakana) ya kudumu ambapo itajengwa chererezo yenye uwezo kubeba meli ya uzito tani 5000, Ujenzi wa meli ya kubeba mizigo yenye uwezo wa kubeba Tani 3500 Ziwa Tanganyika ambayo ni meli kubwa kuliko zote ukanda wa maziwa Makuu, na Ujenzi wa Meli Ziwa Victoria yenye uwezo wa kubeba tani 3000.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa