Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bi. Ester Alexander Mahawe amesema Mwananchi au kikundi chochote kinachokwamisha kujengwa kwa miradi ya Maendeleo ni Wahujumu wa Uchumi na Watachukuliwa hatua kwa mjibu wa Sheria za Nchi
Ameyasema hayo Leo May 26, 2022 katika Mkutano wa hadhara uliofanyikia eneo la Kwizera kata ya Bangwe Manispaa ya Kigoma/Ujiji wakati akiwahutubia Wananchi wa Kata hiyo
Mkuu huyo wa Wilaya amesema wapo Viongozi wa Kisiasa ambao wanawahamasisha Wananchi kugomea miradi inayotarajiwa kujengwa katika Manispaa hiyo kwa maslahi binafsi ikiwemo mradi wa Ujenzi Mwalo wa Katonga na Ujenzi wa Soko la Mwanga Kisasa inayotarajiwa kuanza kujengwa mapema mwezi July , 2022
Kiongozi huyo amesema watu hao hawatavumiliwa na watachukuliwa hatua za Kinidhamu kwa mjibu wa Sheria za Nchi huku akisema taarifa za wanaochochea migomo ya kutopisha ujenzi tayari taarifa zao zipo ofsini kwake na vyombo vya Ulinzi na usalama vinaendelea kuwabaini
Aidha Mkuu huyo wa Wilaya amewaambia wakazi wa Kata ya Bangwe kujengwa kwa Mwalo wa Katonga kutasaidia kuwa na soko la Uhakika la Mazao ya Uvuvi , kuwa na Miundombinu ya kisasa ya ukaushaji mazao ya Uvuvi kwa nyakati zozote za hali ya hewa, kuongezeka kwa ajira katika mwalo huo ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mzunguko wa fedha kwa Wananchi
Amehitimisha kwa kuwataka Wananchi kujiandaa na kuwa tayari kuhesabiwa katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agost 23, Mwaka huu na kuendelea kutunza miundombinu ya Anwani za Makazi inayoendelea kusimikwa katika mitaa mbalimbali
Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma Raphael Msela amewataka Wananchi kujali Miradi inayotekelezwa kutokana na Manufaa yao na kuunda vikundi vya Ulinzi shirikishi ili kuepukana na Vitendo viovu visivyofaa ndani ya jamii
Mkuu wa idara ya Mipango na Uchumi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi amesema Serikali imeendelea kutekeleza Miradi mbalimbali ya Maendeleo kupitia fedha za Serikali kuu na Mapato ya Ndani huku akiwataka Wananchi kuilinda na kuitunza na kuendelea kuwanufaisha jamii kubwa
Mkuu huyo wa Idara amewataka wafanyabiashara wa Soko la Mwanga na Wachuuzi wa Mwalo wa Katonga kuendelea kupisha ujenzi wa Miradi hiyo hadi kufikia June 30, kama walivyoarifiwa huku akisema July 1, 2022 ujenzi utakuwa ukianza katika Maeneo hayo
Awali Diwani wa Kata Mhe. Khamis Said Betse hiyo amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kupeleka fedha katika Kata hiyo kwa lengo la kutekeleza miradi ya Maendeleo tayari Ofisi ya Kata imepokea fedha za awali kiasi cha Million sabini na tano ( Tsh 75, 000,000/=) kwa lengo la ujenzi wa Zahanati Mpya kutokana na Zahanati iliyopo Kata hiyo kutengwa kwa ajili ya kuhudumia magonjwa mlipuko
Ameendelea kusema tayari zaidi ya Billion Moja zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Tanki la Maji litakalohudumia wakazi wa Kata hiyo na Kata zingine ambao wamekuwa wakikabiliana na Changamoto za Maji huku akisema Mamlaka ya Maji Kigoma (KUWASA ) wamelaza mabomba eneo la kiziwani ili kuwahudumia Wananchi wa eneo hilo
Aidha ameitaka kamati ya Ulinzi na usalama ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya kuwachukulia hatua za kisheria wale wanaokwamisha ujenzi wa miradi ya Maendeleo katika Manispaa hiyo
Nao baadhi ya Wananchi waliohudhuria Mkutano huo akiwemo Bi. Getruda Ezron na William Leonard wameipongeza Serikali kwa Miradi inayoendelea kutekelezwa huku Wakisema kujengwa kwa Mwalo wa Katonga kutainua uchumi wa Wananchi na kupandisha thamani ya ardhi ya Kata ya Bangwe
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa