Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ndugu. Salum Hamis Kali amewataka Wanaume kushirikiana na Wanawake (Wake) katika zoezi la uandikishaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa Watoto wa chini ya Umri mitano (05).
Wito huo aliutoa Jana Octoba 09, 2023 katika uzinduzi wa Ugawaji wa vyeti vya kuzaliwa bure kwa Watoto chini ya umri wa miaka mitano (5) Manispaa ya Kigoma/Ujiji uliofanyikia Ofisi ya Kata ya Katubuka.
Katika uzinduzi huo alisema Wanawake wameonekana kuwa wengi ukilinganisha na idadi ya Wanaume wanaoshiriki katika kuandikisha Watoto wao ili kupata vyeti vya kuzaliwa huku akiwataka Wanaume kutoa ushirikiano kwa Wanawake katika zoezi hilo.
Awali akiwasilisha taarifa kwa niaba ya Mkuruģenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Mkuu wa idara ya Mipango, Uratibu na Uchumi Ndugu. Frednand Filimbi alisema tayari zaidi ya Watoto elfu nne Mia tano wameandikishwa tangu zoezi kuanza
Alisema zoezi la utoaji wa vyeti vya kuzaliwa chini ya Umri wa Miaka mitano (05) linaendelea katika Ofisi za Watendaji Kata na Katika vituo vya kutolea huduma za afya.
Zoezi la utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa Watoto chini ya miaka mitano (05) lilizinduliwa Mkoani Kigoma na Waziri wa Katiba na Sheria Nchini Tanzania Dr. Pindi Chana Octoba 03, 2023 katika Uwanja wa Mwanga Community Centre na cheti cha kuzaliwa ni haki ya Mtoto, ni utambulisho wa kwanza wa Mtoto, na kumwezesha kupata elimu na Maisha bora.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa