Na Mwandishi Wetu
Wanawake wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wametakiwa kuchangamkia fursa za kiuchumi zilipo na kufanya kazi kwa bidii ili kuepuka utegemezi.
Ameyasema hayo Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Deodatus Nenze kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake yaliyofanyikia Leo March 06, 2024 katika Uwanja wa Mwanga Community Centre.
Licha ya kufanya kazi kwa bidii Kiongozi huyo amewataka kuendelea kuzingatia malezi ya Watoto katika kuhakikisha kunakuwa na jamii yenye ustawi.
Amewataka Wanawake kuendelea kutoa ushirikiano katika kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa Mamlaka zinazohusika pindi vinapotokea ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Awali akiwasilisha Taarifa Mratibu wa Dawati la Jinsia Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Bernadetha Ntembeje amesema Manispaa hiyo imekuwa ikitoa elimu kwa jami juu ya Umuhimu wa kuwekeza kwa Wanawake ili kuleta maendeleo kwa Taifa, kupambana na Vitendo vya Ukatili , Kusaidia Wanawake katika masuala ya Kisheria, na kushirikiana na Wadau wa Msaada wa Kisheria ili kutambua haki na Wajibu katika kuleta maendeleo ya Jamii.
Kauli Mbiu ya Mwaka huu " Wekeza kwa Wanawake, Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa