Na Mwandishi Wetu
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Bi. Mwantum Mgonja Leo May 03, 2024 amekabidhi vyeti vya ushiriki wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa Mwaka 2022 Kwa Watendaji wa Kata.
Vyeti hivyo vimekabidhiwa Leo May 03, 2024 katika Ukumbi wa Manispaa huku akitoa maelekezo ya Vyeti vyote kugawiwa kwa Walioshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi hadi kufikia Siku ya Jumapili May 05, 2024.
Vyeti hivyo vimetolewa na Ofisi ya Takwimu (NBS) Nchini kwa lengo la kutambua mchango wa Washiriki na kufanikisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika Mwaka 2022.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa