Na Mwandishi Wetu
Wataalamu wa Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Kigoma Jana Oktoba 21, 2025 walikutana kwa mafunzo ya Siku moja (01) kwa lengo la kujifunza namna ya udhibiti na kutokomeza ukatili wa Watoto mtandaoni.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mkuu wa Mkoa yakifadhiliwa na Shirika la kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) yalihudhuriwa na Wakuu wa Idara na Vitengo Mkoa, Maafisa Ustawi wa Jamii, Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa wa Jeshi la Polisi, na Maafisa wa Mahakama.
Akifungua kikao hicho kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa, Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Kigoma Ndugu. Anzuruni Msafiri aliitaka Jamii, Wazazi na walezi kudhibiti na kuwaelimisha Watoto madhara ya ukatili yatokanayo na Matumizi ya vifaa vya kidigitali licha ya faida zake ikiwemo ujifunzaji wa masomo ya kitaaluma.
Aidha aliwataka Washiriki wa mafunzo hayo kuwa mabalozi na wafundishaji wa Jamii katika kupambana na vitendo vya ukatili ndani ya jamii.
Akiwasilisha katika Kikao hicho Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kigoma Ndugu. Petro Mbwaji alisema ukatili wa mtandao ni ukatili unaofanyika kupitia Mitandao ya kidigitali na teknolojia ya Mawasiliano kutokana na matumizi ya vifaa vya kielekroniki kama vile Simu ya mkononi, kompyuta, Saa janja, na Runinga.
Alisema Watoto wanaotumia Mitandao ya kidigitali katika umri mdogo wamekuwa wakikutana na athari hasi kama vile kuanza ngono katika umri mdogo, uraibu wa kutumia mda mwingi Mtandaoni, na kuongezeka kwa mmmonyoko wa Maadili.
Aliendelea kusema licha ya faida za Mitandao ikiwemo Kujifunza mambo na ujuzi mpya, kutazama video za kufurahisha nakusikiliza mziki,Wazazi wanalojukumu la kuwalinda Watoto kwa Kujenga uhusiano mzuri na mtoto kuhusu Matumizi ya TEHAMA, kumuuelimisha na kumtia moyo kutumia mtandao kwa usahihi bila vitisho.
Alisema Jamii lazima ielimishwe ili kuepuka
Udharirishaji wa Watoto kingono kupitia picha, video na vitabu vya katuni ili kuendelea kulinda Maadili ya Kitanzania.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa