Na mwandishi wetu
Wataalamu wa afya halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji jana April 14 waliapa kiapo cha Maadili kutokana na kuteuliwa kwa waganga wafawidhi katika vituo vya afya ili kukuza utendaji kazi na watumishi wengine kubadilishiwa vitengo kiapo hicho waliapa katika ukumbi wa halmashauri chini ya Mwanasheria wa Manispaa Ndugu. Emmanuel Mkwe ,
Akielezea sababu ya mabadiliko hayo Mganga Mkuu wa halmashauri hiyo Dr. Peter Nsanya alisema mabadiliko hayo yalifanyika baada ya baadhi ya vitengo vya idara ya afya kuwa na watu wachache na kuzidiwa katika majukumu yao.
Aliendelea kusema katika mabadiliko hayo yaliyofanyika waganga wafawidhi wa vituo vya afya(viongozi wa vituo) wahakikishe wanasimamia majukumu ipasavyo kwa kufuata utaratibu wa kutoka na kuingia kazini kwa mda uliopangwa na wahakikishe wana toa taarifa kwa walio chini yao pindi wanapokuwa wanadharura katika vituo vyao vya afya.
Naye kaimu afisa utumishi wa halmashauri hiyo Ndugu. Iddi Kalingoji akiwakumbusha wajibu wa watumishi hao alisisitiza juu ya maadili kazini katika utendaji kazi kwa kutoa huduma iliyokusudiwa kwa kumbuka sheria zinazoongoza utumishi wa Umma.
Aliendelea kuwambusha sheria ya utumishi wa Umma Namba 8 ya mwaka 2002 na sheria Namba 6 ya Mwaka 2004 kuhakikisha inatekelezwa ipasavyo ikiwa adhabu yake ni pamoja na kufukuzwa kazini, kushushwa cheo na kupunguziwa mshahara.
Aliendelea kuwasisitiza kuwa waadilifu kazini kufika kwa wakati, kuepukana na ulevi kazini, matumizi ya ofisi ya umma katika shughuli binafsi, kuwa nje ya kazi bila taarifa pamoja na kutoa siri za ofsi ikiwa ni kuvunja sheria.
Naye Mwanasheria wa Manispaa hiyo Ndugu. Emmanuel Mkwe aliwasisitiza watumishi hao kutekeleza majukumu bila kuvunja sheria na kuwaasa kuwa na utamaduni wa kusoma sheria zinazo wahusu wawapo kazini na kueleza kiapo walichoapa ni agano pamoja na Mwajiri wao ambaye ni halmashauri na kuvunja kiapo hicho ni kuvunja mkataba na Mwajiri huyo.
Akieleza kwa niaba ya wataalamu wa Afya Dr. Ramadhani Kahana kutoka dispensari ya Kigoma alisema kiapo walichokiapa ni agano na watahakikisha wanatekeleza majukumu waliyoaswa na kaimu afisa utumishi pamoja na mwanasheria wa halmashauri hiyo huku akiwataka wataalamu wengine kufikisha maagizo waliyoyapata kwa wataalamu waliopo chini yao.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa