Na Mwandishi Wetu
Wazazi wenye watoto chini ya miaka mitano (5) Wilaya ya Kigoma wametakiwa kushiriki zoezi la utoaji chanjo ya Ugonjwa wa Polio inayotarajia kutolewa kuanzia Novemba 17-20, 2022
Ameyasema hayo Katibu Tarafa Ndugu. Maximilian Cyrilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma wakati akifungua kikao cha afya msingi cha Wilaya hiyo kilichofanyika Leo Novemba 15, 2022 katika ukumbi wa Redcross kwa lengo la kuwajengea uelewa wajumbe wa kikao na Kushiriki katika uelimishaji katika zoezi la Utoaji chanjo
Kiongozi huyo amewataka Wazazi na Walezi kutoa ushirikiano kwa timu za wachanjaji watakapofika na kupita nyumba kwa nyumba na katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ili jamii kuepukana na athari zitokanazo na ugonjwa wa polio
Mratibu wa Chanjo Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Waziri Shabani Ramadhani awali akiwasilisha taarifa amesema Ugonjwa wa Polio unaosababishwa na kirusi ambacho huambukizwa kutoka kwa mtu aliyeathirika kwenda kwa mwingine kwa kula au kunywa kitu kilichochafuliwa na kinyesi chenye virusi vya Polio
Ameendelea kusema virusi vya Polio vinapoingia mwilini huathiri mfumo wa fahamu na kusababisha madhara kiafya ikiwa ni pamoja na kupooza kwa ghafla kwa kiungo au viungo na hata kupelekea kifo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa