Na Mwandishi Wetu
Mafunzo ya Uhamasishaji wa Watoto wenye Umri wa Miaka 7-14 Wasio kuwa Shule kwa sababu mbalimbali yameanza leo March 03, 2023 kwa lengo la kurudi Shuleni katika Shule za Msingi
Mafunzo hayo yanatarajiwa kufanyika kwa Siku tatu (03) Katika taasisi ya Ahlulbayt Islamic Centre yakihusisha Maafisa elimu, Wenyeviti wa Serikali Mitaa, Watendaji wa Mitaa na Waelimishaji jamii wa Kata ya Kasimbu na Kibirizi yakifadhiliwa na Shirika la UNICEF
Akifungua Mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Frednand Filimbi amewataka Washiriki Kuzingatia mafunzo ili kuhakikisha jamii inahamasika katika kuwapeleka Watoto kupata elimu
Amesema Manispaa hiyo itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali, Viongozi ngazi ya Kata, Mitaa na jamii katika kuwabainisha Watoto wasiopata elimu kwa sababu ya Utoro, Kuacha Shule na sababu zinginezo wanarudi Shule pasipo kikwazo chochote
Mwezeshaji na Mkufunzi wa Mafunzo hayo ambaye pia ni Afisa Elimu Watu Wazima Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Cornel Kisinga amesema mafunzo haya yanalenga kuwafikia zaidi ya Watoto elfu sita (6000) hadi kufikia Mwaka 2024 wenye Umri wa Miaka 7-14 ambao hawakuwahi Kusoma, utoro na Sababu zingine
Amesema Watoto wenye Umri Miaka saba (07) wataandikishwa katika Mfumo rasmi na uandikishaji wa Watoto wenye Umri wa Miaka 8-14 katika masomo ya MEMKWA yanayomlenga Mwanafunzi kujua Kusoma, Kuandika na kuhesabu na baadae kuingia katika Mfumo rasmi
Amewataka Wazazi, Walezi na Jamii kuwapeleka Watoto katika Shule za Serikali na Kusema elimu hii inatolewa bure bila malipo
Mhudumu ngazi ya Jamii kutoka Kata ya Kibirizi Bi. Yasinta Vitus amesema ndani ya Jamii kumekuwa na Wazazi wanaowatumikisha Watoto wao katika shughuli za Uzalishaji na ajira zisizo rasmi hali inayoathiri mtoto kutoandikishwa na Wengine kuacha kuendelea na Masomo
Amesema wataendelea kuielimisha na kuihamasisha jamii katika kushirikiana kuibua Watoto wasiopata elimu na kuhakikisha wanaandikishwa katika kuanza masomo
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa