Na Mwandishi Wetu
Watumishi wa manispaa ya kigoma/Ujiji wametakiwa kutumia kanuni na misingi ya Maadili ya utumishi wa Umma katika kuwahudumia Wananchi.
Takwa hilo lilitolewa Jana Januari 22, 2026 na Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora katika Mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo.
Akizungumza katika mafunzo hayo Afisa Rasilimali Watu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi na Utawala Bora Bi. Saada Ibrahim alisema Taasisi za Umma zimeundwa kwa ajili ya Ustawi wa Wananchi.
Aliwataka Watumishi kuzingatia kanuni na maadili katika kutoa huduma kwa Wananchi ikiwemo kutoa huduma bora, bidii ya Kazi, kufanya kazi kwa uadilifu, na kuheshimu Sheria.
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Lawi Kajanja aliwapongeza Wataalamu hao huku akisema mafunzo hayo yataendelea kukuza weredi wa Watumishi katika kuendelea kuwahudumia Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa