Na Mwandishi Wetu
Wazazi na Walezi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji wametakiwa kuzungumza na Watoto wao kwa kuwapatia elimu ya kupinga vitendo vya ukatili pamoja na utoaji taarifa ili hatua za kisheria kuchukuliwa
Nasaha hizo zimetolewa Leo June 15, 2023 na Mkuu wa dawati la jinsia na Watoto Mkoani Kigoma Inspecta Maiko Mjema katika Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika Manispaa ya Kigoma/Ujiji katika viwanja wa shule ya Sekondari Katubuka
Katika Maadhimisho hayo amewataka Wazazi, Walezi na Jamii kuwalinda watoto kwa kuwaepusha maeneo hatarishi yanayoweza chochea vitendo vya ukatili kwa jamii
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi, Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu. Deodatus Nenze amesema serikali itaendelea kushirikiana na Wadau mbalimbali ili kuendelea kutokomeza vitendo vya ukatili kwa kuzingatia Sera, Miongozo na kanuni zinazotoa haki kwa Watoto
Amesema Halmashauri imepanga kufanya Shindano la kuibua vipaji vya watoto ili kuhakikisha malengo yao yanafikiwa
Ameendelea kusema tayari mabaraza ya kushughulikia Masuala ya watoto tayari yameundwa kwa kata zote kumi na tisa (19) na mitaa Sitini na nane (68), na Uanzisha kituo cha huduma ya watoto (One stop centre) Hospitali ya Rufaa Mkoani Kigoma Maweni
Maadhimisho hayo yamefanyika yakihusisha Michezo ya kucheza mziki, Uvutaji Kamba, Maigizo na kukimbiza Kuku
Maadhimisho haya hufanyika June 16, kila mwaka na Kauli Mbiu ya Mwaka huu ni Zingatia usalama wa Mtoto katika ulimwengu wa Kidigitali
Endelea kutufatilia kwa kubofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa