Uongozi wa manispaa ya kigoma ujiji chini ya meya Hussein Ruhava na kaimu mkurugenzi Brown Nziku june 8, wamesaini mkataba wa ujenzi wa barabara na mitalo takribani kilomita 12 itakayogharimu shilingi billion 18.6. iliyotolewa na banki ya dunia(WORLD BANK)
Mkataba huo uliosainiwa katika ukumbi wa manispaa ya Kigoma Ujiji ukiongozwa na meya wa manispaa pamoja na aliyekaimu ofsi ya mkurugenzi ndugu Brown Nziku, na viongozi mbalimbali waliohudhulia wakiwemo wakuu wa idara wa halmashauri hiyo wamesaini mkataba huo na kampuni ya kichina ijulikanayo kwa jina la China Railway 15th Bureau Group Corparation, akifungua mkutano huo kaimu mkurugenzi aliwakaribisha waliohudhulia na kusema mkataba huo unaenda kuleta mapinduzi makubwa ya kimaendeleo kwa upande miundombinu jambo litakalo pelekea mazingira kuwa safi na manispaa kuendelea kupaa katika viwango vya kupendeza.
Naye meya wa manispaa Hussein Ruhava akihutubia mkutano huo ametoa pongezi zake kwa serikali na kumpongeza waziri wa TAMISEMI mstaafu mhe. Simba chawene na kutoa pongezi kwa katibu wa TAMISEMI ndugu Mussa Iyombe pamoja na kwa uongozi wa mkoa, benki ya NMB TANZANIA na tawi la Kigoma kwa ushirikiano mzuri wa kufanikisha halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji kufanikisha halmashauri inapata mkopo chini ya usimamizi Tanzania Strategic Cities Project(TSCP)
Meya huyo aliendelea kwa kusema ujenzi huo utaleta mafanikio makubwa ikiwemo ajira kwa wakazi wa manispaa, uboreshaji wa mazingira pamoja na manispaa hiyo kuelekea kuwa hadhi ya jiji , ameendelea kusema kata zitakazopitiwa na ujenzi huo ni kata tisa na kufafanu barabara zitakazojengwa ni pamoja na barabara ya msikiti wa Kigoma hadi Mwembetogwa, barabara ya Ujenzi sido hadi Nazareth, barabara ya Kagashe hadi katubuka , barabara ya Maweni hadi Burega , barabara ya Tanesco, press club hadi Kigoma shule ya msingi, mfereji wa Mlole hadi Gungu na mfereji wa Kasimbu, machinjioni .
Aidha meya huyo ameendelea kuwataka waandishi wa habari kuhabarisha jamii ya kigoma kuwataka wakazi wa mkoa wa kigoma kutoa ushirikiano kwa wakandarasi hao , na kuwataka wakazi kutunza miundombinu inayojengwa na inayoendelea kujengwa.
Naye Sun Jinlan mwakilishi wa kampuni hiyo ya China Railway 15th Bureau Group Corporation amesema ujenzi huo utafanyika kwa uzuri kwa mjibu wa mkataba uliosainiwa wa kujenga kiwango cha lami nzito, na kusema mkataba huo unatarajiwa kutekelezwa ndani ya miezi kumi na tano. Ameendelea kusema kampuni hiyo inauzoefu wa ujenzi hapa nchini na kusema kampuni hiyo imeweza kujenga daraja la Kilombelo na Magufuli bridge.
Aidha mkutano huo umehitimishwa kwa kusainiana mkataba huo na pamoja na kupiga picha za pamoja kwa Meya wa Manispaa, kaimu mkurugenzi , wakuu wa idara pamoja na madiwani.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa