Waziri wa TAMISEMI Sulemani Japho leo January 4, ameanza ziara yake mkoani Kigoma katika halmashauri ya Kigoma/Ujiji kwa kukagua kituo cha biashara na barabara zinazoendelea kujengwa na zilizokamilika.
Katika ziara yake iliyoanzia katika barabara ya kakolwa inayojengwa na Tanzania Strategic Cities Project (TSCP) kwa ufadhili wa benki ya dunia (WB)kwa kukagua jinsi inavyoendelea kujengwa na kuridhika na ujenzi huo na baada ya hapo msafara wa Waziri huo ulielekea katika kituo cha biashara kilichopo katika halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Akitoa taarifa kaimu Afisa Biashara Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndg. Festo Nashoni amesema kituo kilikamilika ujenzi tangu mwezi wa 6,2018 kwa gharama ya shilingi za Kitanzania milioni hamsini na tatu laki tisa sabini na sita na mia nne( Tsh 53976400) ambapo ameeleza watu wanaopaswa kufanyia katika jengo hilo ni Afisa TRA Kigoma, Afisa biashara Manispaa ya Kigoma Ujiji, Afisa biashara halmashauri ya wilaya ya Kigoma, Afisa kutoka Uhamiaji na mawakala wa benki.
Ameendelea kusema licha ya jengo kukamilika na wao kufanya kazi katika jengo hilo tayari wameshawataarifu kwa barua wadau wote kwa lengo la kuja kufanya kazi lakini bado hakuna ambaye tayaria ameshafika kuja kufanyia kazi katika eneo hilo jambo linalosababibisha wafanyabishara kutumia gharama kubwa na mda mwingi katika kukamilisha shughuli zao katika ofsi hizo zinazotegemeana kiutendaji.
Naye waziri huyo waTAMISEMI Sulemani Japho akiwa katika kituo hicho amepongeza halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa kukamilisha ujenzi wa kituo hicho licha ya kutilia shaka gharama zilizotumika katika ujenzi wa jengo hilo.
Ameendelea kuwatia moyo watumishi wa ofsi ya biashara Manispaa ya Kigoma/Ujiji kufanya kazi kwa uzuri kwa kuhakikisha mapato ya serikali hayapotei na kuahidi kuwasilisha suala la TRA Kigoma kwa Waziri wa fedha na mipango kushindwa kupeleka watumishi katika jengo hilo jambo linalosababisha kudolola kwa shughuli za lengo la ujenzi wa kituo hicho.
Waziri huyo amemtaka Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji kuhakikisha watumishi waliopo katika halmashauri yake ambao hawajaenda kufanyia kazi katika kituo hicho wahakikishe wanaanza kazi mara moja na kumtaka kuhakikisha kituo kinafanya kazi katika hali ya uzuri.
Baada ya hapo waziri huyo alihitimisha ziara yake kwa kukagua barabara ya Rusimbi ambayo tayari imeshakamilika na kukagua barabara ya Ujiji-Kagera ambapo amelizishwa na ujenzi unaoendelea.
Waziri huyo yupo ziarani Mkoani Kigoma kwa siku nne ambapo atatembelea miradi mbalimbali mkoani humo katika wilaya ya Buhigwe, Kasulu na Kakonko ambapo atetembelea kituo cha biashara pia.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa