Na Mwandishi Wetu
Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha na kusogeza huduma za Matibabu karibu na Wananchi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Jumamosi June 21, 2025 Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Mhe. Kilumbe Shabani Ng'enda alizindua Zahanati Mpya Mbili (02) kwa lengo la kuanza kutoa huduma katika Zahanati ya Kibirizi na Zahanati ya Kitongoni.
Akitoa taarifa Wakazi wa ufunguzi wa Zahanati hizo, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Dr. Hashim Mvogogo alisema ujenzi wa Zahanati ya Kibirizi umegharimu kiasi cha fedha za Kitanzania Millioni 109, na Zahanati ya Kitongoni Kiasi cha fedha za Kitanzania Millioni 143 huku vifaa tiba vikigharimu kiasi cha fedha za Kitanzania Million 50 kwa Zahanati zote mbili.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa