Na Mwandishi Wetu
Baraza la Madiwani Manispaa ya Kigoma/Ujiji Leo January 21, 2025 limejadili na kupitisha rasmu ya bajeti inayotarajiwa kutekelezwa kwa Mwaka wa fedha 2025/2026 kwa kukusanya na kutumia kiasi cha fedha za Kitanzania Tsh 42, 724, 317,968.00.
Baraza limefanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo likiongozwa na Naibu Meya Mhe. Mgeni Kakolwa ambapo awali akiwasilisha taarifa Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Kisena Mabuba amesema kiasi cha fedha za Kitanzania 5,232,158,096.00 ni fedha za zinazotarajiwa kukusanywa kutoka vyanzo vya Mapato vya ndani.
Amesema Manispaa hiyo imepandisha makisio ya bajeti ya Mapato ya ndani kwa zaidi ya asilimia 30 kutoka Billion 4.01 kwa Mwaka 2024/2025 hadi Billion 5. 2 Sawa na ongezeko la zaidi ya billion moja (1, 220,576,096/=)
Amesema kiasi cha fedha za Kitanzania 9,996,616,000/= ni ruzuku kutoka Serikali Kuu kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo ongezeko la bajeti yote ni kwa 3% ukilinganisha na bajeti ya 2024/2025.
Rasimu ya mpango na bajeti iliyopitishwa kwa Mwaka 2025/2026 imeandaliwa kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020- 2025, Malengo ya maendeleo endelevu (SDGs), Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Taifa 2025 , Sheria ya Bajeti Na. 11 ya Mwaka 2015 sura ya 349, Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (05) 2021- 2026, Mpango Mkakati wa Halmashauri na Maelekezo na ahadi mbalimbali za Viongozi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa