Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua Leo Septemba 25, 2025 amekabidhi hundi ya mikopo isiyokuwa na riba ya 10% kwa vikundi 58 vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu yenye thamani ya fedha za Kitanzania zaidi ya Millioni Mia Tano (Tsh 555,652,400/=) Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Amekabidhi hundi hiyo katika mafunzo kwa Wanachama wa vikundi hivyo yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa Kushirikiana na Benki ya CRDB yaliyofanyikia ukumbi wa Joy Harvest.
Amewataka Wanachama wa Vikundi hivyo kutumia Mikopo kwa malengo yaliyokusudiwa kwa kuzalisha kulingana na shughuli wanazozitekeleza ili kuwanufaisha, kuzirejesha kwa wakati na kunufaisha makundi mengine.
Akitoa taarifa katika mafunzo hayo Mratibu wa Mikopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Jabir Majira amesema kwa awamu hii ya pili ya utoaji ikopo jumla ya vikundi 58 vimenufaika na mkopo usiokuwa na riba wa fedha za Kitanzania zaidi ya Million Mia Tano (Tsh 555,652,400/=) Vikundi vya wanawake vikiwa 40, Vijana 15, watu wenye Ulemavu 03 kutoka katika Kata 19 za Manispaa hiyo.
Amesema katika mafunzo hayo Wanachama hao watajengewa uwezo namna kusimamia fedha na uwekaji akiba, usimamizi na uendeshaji wa vikundi, usimamizi wa Masoko, utunzaji wa kumbukumbu, na fursa za Manunuzi ya Umma kwa Vikundi.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa