Na Mwandishi Wetu
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi Manispaa ya Kigoma/Ujiji wametakiwa kusimamia Walimu na kutumia mfumo wa kielektroniki katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji Mashuleni
Ushauri huo umetolewa na Mkufunzi wa Mafunzo hayo Ndugu. Backer Hebron katika mafunzo ya Mpango endelevu wa Walimu kazini (MEWAKA) yaliyofanyikia katika Shule ya Msingi Kabingo Leo Septemba 26, 2022 yakiandaliwa na Mradi wa Shule bora unafadhiliwa na mfuko wa UK aids
Katika mafunzo hayo Walimu hao wametakiwa kutumia mfumo wa kielekronic Learning Management System (LMS) na Maktaba Mtandao katika kujisomea, kupakua vitabu, kupakua miongozo ya kielimu, na tathimini ya mahitaji ya elimu
Mkufunzi huyo ameendelea kuwataka Walimu kuwa wabunifu katika suala la Ufundishaji huku wakizingatia matumizi sahihi ya mifumo ya Tehama itakayosaidia suala la Ulinzi na Usalama wa Mazingira kwa kuepuka uchafuzi na uzalishaji wa Karatasi
Aidha katika mafunzo hayo walimu hao wamesisitizwa kuzingatia elimu jumuishi inayozingatia uboreshaji wa Mazingira yatakayosaidia Wanafunzi wenye ulemavu na Wanafunzi wa kike kujifunza katika mazingira bora na salama
Miradi wa Shule bora unatekelezwa katika Mikoa tisa (9) Nchini Tanzania ukihusisha Halmashauri sitini na saba (67) na Shule elfu tano mia saba hamsini na saba ( 5, 757) na Unatarajia kuwanufaisha Wanafunzi zaidi ya Milioni tatu na laki nane ( 3, 800,000) na Walimu zaidi ya elfu hamsini na nne ( 54, 000)
Mikoa inayotekeleza mradi wa Shule bora ni pamoja na Mkoa wa Kigoma, Katavi, Dodoma, Mara, Pwani, Rukwa, Simiyu, Singida na Mkoa wa Tanga
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa