Na Mwandishi Wetu
Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kigoma Mjini Ndugu. David Rwazo amewataka wasimamizi wa vituo kuzingatia Sheria za Uchaguzi na kutoa haki Sawa kwa Wapiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge na madiwani.
Ameyasema hayo alipokuwa akifungua mafunzo ya Siku mbili (02) kwa wasimamizi wa vituo yanayofanyika ukumbi wa Angrikana Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Amewataka kufuata taratibu mbalimbali za kikatiba na Kisheria ambazo ndizo Msingi wa Uchaguzi huru na wa haki.
Aidha amewataka kusoma Katiba, Sheria, kanuni, miongozo na maelekezo mbalimbali yatakayotolewa na Tume ili kurahisisha Utekelezaji wa Kazi za Uchaguzi.
Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Jumatano Oktoba 29, 2025.
#kurayakohakiyakojitokezekupigakura
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa