Na Mwandishi Wetu
Zoezi kusasisha, kuhuisha na kukusanya taarifa mpya za Anwani za makazi limeanza Leo March 15, 2024 katika Kata na Mitaa mbalimbali za Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Zoezi hilo limeanza likifanyika na Watendaji wa Mitaa kwa kupita katika Makazi, maeneo ya biashara na Umma kwa kuhakiki na ukusanyaji wa taarifa mpya.
Zoezi hilo linafanyika likisimamiwa na Wataalamu wa Mfumo wa Anwani za Makazi kutoka Wizara ya habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari likihusisha Utambuzi na uwekaji wa Anwani za makazi (namba ya jengo, au kiwanja), majina ya barabara na postikodi.
Zoezi hilo linafanya kila Mtanzania kuwa na anwani halisi ya Makazi yatakayosaidia kila mtu kupatikana kirahisi, utambulisho wa watu, usajili wa biashara, kufanyika kwa biashara mtandaoni ambapo Wafanyabiashara na wanunuzi watakuwa na uwezo wa kununua na kumfikishia mteja bidhaa, upatikanaji wa huduma za dharura kama vile polisi, na huduma za zima moto.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz @nzotamganwa @wizarahmth @napennauye @ortamisemi
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa