Na Mwandishi Wetu
Manispaa ya Kigoma/Ujiji imeanza zoezi la upimaji na kuwabaini Wanafunzi wa Shule za Sekondari wenye changamoto ya kutokusikia (uziwi)
Zoezi hilo limeanza Leo April 05, 2023 kwa Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Buronge na Masanga kwa lengo la kuwatambua ili kubaini mbinu za ufundishaji na kuinua ufaulu katika masomo yao
Zoezi hilo limefanyika kwa kupima uwezo wa usikivu wao likihusisha uwepo wa Wazazi na Walezi ili kupata elimu namna ya kuishi nao na kupinga vitendo vya ukatili
Mtaalamu wa kuhudumia wenye Matatizo ya kutokusikia na Mwalimu. Titus Rubundi Hamis katika zoezi hilo amesema changamoto ya Kutokusikia na Uziwi kunachangiwa na kuugua mda mrefu mara kwa mara na matumizi ya dawa kali kwa Watoto, na matibabu yasiyo rasmi
Amewataka Wazazi na Walezi kukaa na Watoto wao mara kwa mara na kubaini changamoto zao kupitia michezo na malezi ya kila siku ili kupatiwa matibabu mapema kabla ya kukua kwa tatizo
Afisa elimu Maalumu Sekondari Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Shingwa Hamisi Shingwa anasema Wanafunzi wenye changamoto za ulemavu wanakutana na changamoto ya kutengwa na kuwa wapweke hali inayoweza kusababisha kushuka kwa taaluma
Amesema elimu imeendelea kutolewa kuhusiana na elimu jumuishi ikiwemo ujenzi miundombunu sahihi ili kuhakikisha elimu inatolewa kwa usawa
Ameitaka Jamii, Wadau na Taasisi mbalimbali kujitokeza kuwasaidia Wanafunzi na Watoto wenye changamoto ya usikivu (uziwi) kwa kutoa vifaa vya usaidizi wa kusikia ikiwa ni pamoja na ulemavu mwingine
www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa