Na Mwandishi Wetu
Zoezi la kuwarejesha Wanafunzi wenye umri wa Miaka 7-14 walioacha Shule kwa sababu mbalimbali limeanza Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
Zoezi hilo lilianza Jana Januari 15, 2025 ambapo Watendaji wa Mtaa, Waratibu elimu Kata na Wenyeviti wa Serikali wanaendelea kuwatambua Wanafunzi hao kwa kupita katika Kaya na kutoa elimu kwa Watoto na wazazi ikiwa ni pamoja na kubandika mabango ya hamasa ya Wanafunzi kurejea Shuleni.
Zoezi hili linalenga kuwarejesha Wanafunzi Mia tisa sitini na tatu (963) katika Kata za Gungu , Kibirizi , Bangwe , Buhanda, Kasimbu, Kitongoni, Kipampa, Buzebazeba, Mwanga kusini, Mwanga Kaskazini, Kagera, Katubuka, Machinjioni, Majengo na Rubuga.
Zoezi la kuwarejesha Wanafunzi linafanywa na Serikali kwa Kushirikiana na Shirika la Kimataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kutoa vifaa vya Shule kama vile Daftari, kalamu, begi na taulo za kike.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz @uniceftz @unicef
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa