Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Dr. Rashid Chuachua amezindua zoezi ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo Manispaa ya Kigoma.
Uzinduzi huo umefanyika Leo Februari 14, 2024 katika ukumbi wa Redcross kwa kugawa vitambulisho kwa Wafanyabiashara ndogondogo Mia mbili hamsini (250).
Akizindua zoezi hilo Mkuu wa Wilaya amesema vitambulisho hivyo vinawapatia fursa ya kutambulika na taasisi mbalimbali ikiwemo za kifedha katika kujiongezea mtaji, masoko, elimu ya Ujasiriamali, mikopo na huduma mbalimbali.
Aidha amewataka Wajasiriamali hao kutumia fursa ya mikopo ya Halmashauri na kutumia Wataalamu waliopo katika kupata mafunzo na elimu mbalimbali.
Akizungumza katika hafla hiyo Kaimu Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii Ndugu. Majira Jabir amesema zoezi la utambuzi na usajili wa wafanyabiashara ndogondogo katika Manispaa hiyo unaendelea ili kuwanufaisha Wananchi wengi zaidi.
Afisa Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni Mratibu wa Vitambulisho vya wafanyabiashara ndogondogo Manispaa Ndugu. Theonest John Nyabenda amesema vitambulisho hivyo vitawezesha kujua idadi ya Wafanyabiashara na kuwezesha Manispaa kuwa na mpango wa kuendelea kutenga na kuboresha miundombinu rafiki.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa