Na Mwandishi Wetu
Kamisa wa Sensa Nchini Tanzania Mhe. Anne Semamba Makinda amewataka Viongozi Serikali na Kisiasa kupanga Maendeleo kwa kuzingatia takwimu zilizopatikana kutokana na Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwezi Agosti, 2022
Aliyasema hayo katika semina ya Usambazaji na uhamasishaji wa Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 iliyofanyika Jana February 03, 2022 katika Ukumbi wa Kigoma Social hall uliopo Manispaa ya Kigoma/Ujiji
Katika Semina hiyo Waliohudhuria ni pamoja na Sekratrieti ya Mkoa, Waheshimiwa Madiwani wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji, Wakuu wa Idara na Vitengo, Watendaji wa Kata na Mitaa pamoja na Wenyeviti wa Serikali za mitaa
Aliwataka Viongozi kutopanga Maendeleo kwa upendeleo bali kuzingatia takwimu zinazoendelea kutolewa na Serikali kwa Mjibu wa Sensa ya Watu na makazi
Alisema kuwa takwimu za idadi ya Watu, Idadi ya Majengo na anwani za makazi kwa ngazi ya Halmashauri, Kata, Mitaa na Vitongoji zinatarajiwa kutolea mwishoni mwezi February mwaka huu
Aliendelea kusema zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Nchini limefanyika kwa ufanisi katika hatua tatu ikiwa ni elimu na uhamasishaji wa Wananchi kushiriki Sensa , Siku ya Sensa na kwa sasa ipo hatua ya tatu kuandika ripoti na Usambazaji, na uelimishaji wa matumizi ya matokeo ya Sensa
Awali Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Michael Ngayalina alisema takwimu za Sensa zitaendelea kunufaisha makundi mbalimbali ikiwemo makundi ya Wafanyabiashara, Wakulima na vikundi vya wajasiriamali katika kuhakikisha wanapanga mipango yao ya kiuchumi
Aliendelea kusema takwimu za Mkoa zilizopatikana na takwimu za Halmashauri, Kata na Mitaa zinazoendelea kuchambuliwa zitasaidia Serikali kuendelea kupanga mipango ya Maendeleo kwa kuzingatia takwimu na mahitaji ya Wananchi
Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dr. Albina Chuwa, aliwataka viongozi hao wa ngazi ya Halmashauri, Kata na Mitaa kufuatilia takwimu katika maeneo yao pindi zinapokamilika kuzitumia katika kupanga maendeleo katika maeneo yao
Akiwasilisha taarifa Mratibu wa Sensa Taifa Ndugu. Seif kuchengo alisema takwimu za Halmashauri, Kata na Mitaa zinanaendelea kukamilishwa huku akisema kwa mjibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 Watu waliolala Nchini Tanzania ni 61,741,120 huku Waliolala Mkoani Kigoma ni jumla ya Watu 2,470,967 Wanaume Wakiwa 1,186,833 na Wanawake1,284,134
Alihitimisha kwa kusema idadi ya Watu imeongezeka kwa mwaka 2022, sawa na wastani wa ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka (the annual intercensal population growth rate) la asilimia 3.2
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa