Na Mwandishi Wetu
Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi ni Msingi wa Usalama wa Nchi, Ujenzi wa Uchumi na Ustawi kwa Wananchi.
Serikali ya Awamu ya Sita Nchini Tanzania chini ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha Sekta ya Kilimo Manispaa ya Kigoma/Ujiji ili kuongeza tija na kipato kwa Wakulima.
Maafisa ugani kumi na tatu (13) katika Kata za Manispaa ya Kigoma/Ujiji wamepatiwa pikipiki ili kuwafikia Wakulima kwa wakati na tayari Wakulima Mia mbili arobaini na Sita (246) wamepewa mafunzo ya kilimo hifadhi ili kukabiliana na Mabadiliko ya tabia ya Nchi.
Aidha Maafisa ugani kumi na nne (14) wamepatiwa vifaa maalumu vya kupima udongo ili Wakulima waweze kutambua afya ya udongo katika mashamba yao.
Karibu Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane nane) Banda la Manispaa la Manispaa ya Kigoma/Ujiji yanayoendelea Kanda ya Magharibi Manispaa ya Tabora katika Viwanja vya Fatuma Mwasa.
Kauli mbiu ya Mwaka huu 2025 ni "Chagua Viongozi Bora kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi".
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa