Na Mwandishi Wetu
Baraza la biashara Wilaya ya Kigoma limeazimia Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma/Ujiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma kuanzisha vituo kwa ajili ya uuzaji mazao au bidhaa zitokanazo na zao la michikichi.
Azimio hili limejadiliwa katika Baraza la Biashara lililofanyika Leo Novemba 26, 2025 katika ukumbi wa Kigoma Social Hall likiongozwa na Afisa Tawala Bi. Dorah Buzaire kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Kigoma.
Afisa Tawala huyo amesema vituo hivyo vitahusika na uuzaji wa mazao yatokanayo na mnyororo wa thamani wa zao hilo kama vile Mawese, Sabuni na chakula cha mifugo.
Amesema vituo hivyo vitasaidia kuinua zao hilo ambalo ni la kimkakati Mkoani Kigoma ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa masoko ya uhakika na kukuza uchumi wa Wakulima.
Mwenyekiti wa Chemba ya biashara Mkoa wa Kigoma(TCCIA) Ndugu. Obadia Kabuga katika baraza hilo amezitaka tasisi mbalimbali kuwalipa Wafanyabishara (Wazabuni) ambao wamekuwa wakitoa huduma katika miradi na maeneo mbalimbali.
Zaidi bofya www.kigomaujijimc.go.tz
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa