Na mwandishi wetu
Baraza la madiwani la halmashuri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji kupitia Mwenyekiti (Meya) wake Mhe. Hussein Ruhava jana limetoa vinyago kwa shule zilizofanya vibaya katika matokep ya mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na kidato cha nne kwa mwaka 2018.
Meya huyo wa halmashauri ya manispaa ya Kigoma/Ujiji ametoa vinyago hivyo kwa shule za msingi tatu na shule za sekondari tatu baada ya baraza kupokea taarifa kutoka katika kamati ya Uchumi, Elimu na Afya kwa kueleza kuwa shule hizo ndizo zilizoburuza mkia katika matokeo ya kitaifa kwa matokeo ya Halmashauri.
shule zilizofanya vibaya na zilizo pokea vinyago ni shule ya msingi Mnarani, shule ya Msingi Ujiji na shule ya Msingi Businde na kwa shule za sekondari ikiwa ni shule ya sekondari Wakulima, shule ya Sekondari Kirugu na shule ya Sekondari Kasingirima.
Meya huyo aliendelea kusema halmashauri inayomikakati mikubwa ya kuhakikisha taaluma inakuwa na hasa kwa wanafunzi wa kike ambao imebainika wamekuwa wakifanya vibaya katika mitihani hiyo huku akisema tayari kampeni ya kuinua ufaulu wa mwanafunzi wa kike imezinduliwa tangu march 6, mwaka huu.
Aliwataka wadau mbalimbali wa elimu kuendelea kutoa elimu kwa jamii na wanafunzi umuhimu wa elimu hasa kwa watoto wa kike huku akisema halmashauri inatoa zawadi kwa shule na kwa mwanafunzi wa kike anayefanya vizuri kwa matokeo ya mitihani ya Kitaifa.
Akiwasilisha taarifa hiyo Mwenyekiti huyo wa kamati ya Uchumi,Elimu na Afya alisema halmashauri imekuwa ikitoa vinyago hivyo kwa shule zinazofanya vibaya kwa ngazi ya halmashauri kila mwaka jambo ambalo limesababisha halmashauri hiyo kuendelea kushikiria nafasi ya kwanza kwa ngazi ya Mkoa.
Aliendelea kueleza wataendelea kufanya hivyo kutoa vinyago kwa shule zitakazofanya vibaya ili shule hizo wajitahidi zaidi na kuhakikisha wanainua taaluma kwa wanafaunzi na matokeo ya mitihani ya kitaifa na hatimaye halmashauri hiyo kufanya vizuri zaidi katika ngazi ya Taifa.
Katika baraza hilo kamati zingine zilizowasilisha ni kamati ya Mipango miji, Ujenzi na Mazingira na kamati ya Ukimwi ,ambapo kamati ya Mipango miji, Ujenzi na Mazingira chini ya Mwenyekiti Maulidi Kacheche imelipendekeza uanzishwaji wa kampuni ya ujenzi itakayofanya kazi na kuwa na mitambo mbalimbali na kuweza kuingizia halmashauri kipato kutokana na fedha zitakazopatikana.
Meya wa halmashauri hiyo aliahirisha baraza hilo majira ya jioni na kusema baraza hilo litaendelea siku ya jumanne ambapo kamati ya Fedha na Uongozi ndipo itawasilisha taarifa yake.
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa