Na Mwandishi wetu
Viongozi wa vyama na vilabu vya michezo Manispaa ya Kigoma/Ujiji leo April 23, wamekutana na uongozi wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) kwa lengo la kukuza na kuboresha michezo mbalimbali katika Manispaa hiyo
Afisa kutoka Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Ndugu. Edson Ringo amewataka viongozi wa vilabu na vyama vya michezo kuheshimu katiba zao kwa kufanya uchaguzi wa viongozi mara kwa mara kutokana na baadhi ya viongozi wa vyama na Vilabu kungangania madaraka
Aidha ameutaka uongozi wa mpira Mkoa wa Kigoma kutoruhusu vilabu visivyosajiliwa kushiriki mashindano mbalimbali ya michezo kwani kufanya hivyo ni kukiuka kanuni na taratibu huku akiwataka viongozi hao kusajili vilabu na vyama vyao mara moja
Afisa utamaduni na Michezo Manispaa ya Kigoma/Ujiji Ndugu. Abdul Utimbe amewataka viongozi hao kufanya kazi kwa ushirikiano kwa kuhakikisha wanafata sheria na kanuni za uendeshaji wa michezo huku akiwataka viongozi hao kuwa na utamaduni wa kuwasomea wanachama na wanamichezo taarifa mbalimbali za uendeshaji wa vilabu na vyama
Katibu wa Chama cha Mpira Mkoa wa Kigoma(KRFA) Ndugu. Omary Gindi amesema wao kama chama wamekuwa na utamaduni wa kutoa taarifa za chama kwa wanachama wao huku akiwataka baraza la Michezo Tanzania (BMT) kuvisaidia vilabu kwa kuleta mrejesho kutokana na fedha zinazokusanywa kutoka tozo za lango kipindi cha michezo mbalimbali
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa