Na Mwandishi Wetu
Kampeni ya Usafi na Usafi imeendelea leo March 17, 2023 katika mwalo wa Kigodeko ambapo Wakazi wa Kata ya Kigoma wametakiwa kutumia urejereshwaji wa taka zitokanazo na bidhaa za plastiki ili kujiongezea kipato
Ameyasema hayo Mtaalamu kutoka Arena recycling industry Ndugu. Zagalo Emmanuel ambapo amesema utupaji taka ovyo katika vyanzo vya maji hasa plastiki ni hatari kwa mazalia ya Samaki na Samaki
Amesema jamii inapaswa kujifunza elimu rejereshi ili kutumia plastiki katika uzalishaji wa Bustani za majumbani, Maua, ufyatuaji tofali,Vigae na Mapambo ili kutumika katika kujiajiri na katika kujiingizia kipato
Amesema katika kuhakikisha kunakuwa na matumizi sahihi ya Plastiki iliyotumika wanatarajia kutoa mafunzo kwa Wakazi wa Manispaa ya Kigoma/Ujiji kwa lengo la kuwa na ujuzi katika kuhakikisha taka za plasitiki hazitupwi ovyo na kuleta athari katika Ziwa Tanganyika
Serikali imeanzisha kampeni mahususi ya kusafisha fukwe za maziwa makuu ya Tanganyika, Viktoria, na Nyasa kupitia kampeni ya ‘Fukwe safi -Ziwa Salama” yenye lengo la kusafisha na kuondoa taka hasa Plastiki
Taka za plastiki zinapotupwa Ziwani haziozi badala yake huvunjika katika vipande vidogo vidogo ambavyo huweza kuleta athari hasi hasa kwenye mazalia ya Samaki na samaki
Manispaa ya Kigoma Ujiji
Sanduku la Posta: S.L.P 44
Simu: +255 28 2802535
Namba ya Simu: +255765660847
Barua pepe: municipal@kigomaujijimc.go.tz ictsecurity@kigomaujijimc.go.tz
Hakimiliki@2017 Manispaa ya Kigoma Ujiji. Haki Zote Zimehifadhiwa